1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban wadhibiti sehemu kubwa ya mkoa wa Kunduz

8 Agosti 2021

Wapiganaji wa Taliban Jumapili wamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mkoa wa kaskazini mwa Afghanistan wa Kunduz, ikiwemo afisi ya gavana na makao makuu ya polisi, amesema afisa mmoja wa baraza la mkoa huo.

Afghanistan Taliban-Offensive auf Kundus
Picha: Ajmal Kakar/XinHua/dpa/picture alliance

Taliban pia imeteka majengo ya serikali katika mji mkuu wa mkoa wa kaskazini wa Sar-e Pul ambapo wamewafukuza maafisa kutoka mji huo na kuwapeleka katika kambi ya kijeshi, kulingana na Mohammad Noor Rahmani, ambaye ni afisa katika baraza la mkoa huo.

Mwanachama mwengine wa baraza hilo la mkoa Ghulam Rabani Rabani amesema kulikuwa na mapigano kati ya wanamgambo na vikosi vya serikali katika eneo hilo lililo na afisi za serikali na baadae Taliban wakafanikiwa kuteka majengo hayo.

Rabani amesema wamechukua udhibiti wa jengo kuu la gereza la Kunduz. Ameongeza kwamba mapigano yanaendelea katika uwanja wa ndege na sehemu zengine za mji huo.

Wanajeshi wa Afghanistan wakipiga doria mkoa wa KunduzPicha: Ajmal Kakar/Xinhua/imago images

Mji wa kwanza wa mkoa watekwa baada ya miaka kadhaa

Kunduz ni eneo la kimkakati ambalo ni njia ya rahisi ya kufika sehemu zengine za Afghanistan kaskazini pamoja na Mji Mkuu Kabul ulioko umbali wa kilomita 335. Iwapo mkoa wa Kunduz utaanguka basi kundi la Taliban litakuwa limefanikiwa pakubwa na itakuwa ni kama kipimo cha uwezo wao wa kuyateka na kudhibiti maeneo. Kunduz ni mmoja ya miji mikubwa ya Afghanistan ukiwa na idadi jumla ya watu ya zaidi ya 340,000.

Hapo Ijumaa, wanamgambo wa Taliban waliuteka mji mkuu wa kwanza wa mkoa baada ya miaka kadhaa walipochukua udhibiti wa Zaranj, katika mpaka wa nchi hiyo na Irankatika mkoa wa kusini wa Nimroz.

Jumamosi wapiganaji wa Taliban waliingia katika mji mkuu wa mkoa wa Jawzjan baada ya kuteka miji tisa kati ya kumi katika mkoa huo. Miji mingine mikuu ya mikoa 34 nchini humo iko katika hatari pia kwa kuwa Taliban inaiteka miji mingi Afghanistan kwa kasi ya juu mno.

Makao yote makuu ya serikali yako chini ya udhibiti wa Taliban

Huku hayo yakiarifiwa makombora ya angani yameharibu zahanati na shule ya sekondari katika mji mkuu wa mkoa wa kusini wa Helmand, amesema afisa katika baraza la mkoa huo. Taarifa ya wizara ya ulinzi imethibitisha kwamba makombora ya angani yamefanyika katika sehemu kadhaa za mji wa Lashkar Gah. Taarifa hiyo imesema majeshi ya serikali yameyalenga maeneo ya Taliban ambapo wamewauwa wapiganaji 54 na kuwajeruhi 23.

Mapigano makali yamezuka mjini Kabul

00:58

This browser does not support the video element.

"Mapigano makali yalianza jana mchana, makao makuu yote ya serikali yako chini ya udhibiti wa Taliban, ni kambi ya kijeshi tu na uwanja wa ndege ndio ulio chini ya udhibiti wa jeshi la Afghanistan," alisema Amruddin Wali, mbunge katika bunge la mkoa la Kunduz.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema kundi limedhibiti mkoa huo pakubwa na linakaribia kufika katika uwanja wa ndege.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW