1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinara wa shambulio la kujitoa mhanga auliwa Afghanistan

26 Aprili 2023

Operesheni iliyofanywa na kundi la Taliban nchini Afghanistan imewezesha kuuliwa muhusika mkuu aliyefanya shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul mnamo mwaka 2021 ambapo wanajeshi 13 wa Marekani waliuawa.

Afghanistan Kabul | Explosion nahe Innenministerium: Taliban auf Militärfahrzeug
Picha: Ebrahim Noroozi/AP/picture alliance

Serikali ya Taliban nchini Afghanistan imefanya operesheni iliyowezesha kuuliwa mtu anayeaminiwa kuhusika na shambulio la kujitoa mhanga mnamo tarehe 26 Agosti mwaka 2021 katika uwanja wa ndege wa mjini Kabul. Katika shambulio hilo wakati Marekani ilipoamua kujiondoa kutoka nchini Afghanistan, wanajeshi 13 wa Marekani na takriban raia wa Afghanistan170 walikufa.

Umati wa watu waliongia kwenye uwanja wa ndege wa Kabul kujaribu kupata nafasi ya kuondoka Afghanistan 2021.Picha: AP Photo/picture alliance

Hapo awali, Marekani na serikali yaTaliban hazikuwa na uhakika kwamba mtu huyo alikufa au alikuwa bado yupo hai lakini kulingana na maafisa, mtu huyo aliuawa wakati wa mfululizo wa mapigano mapema mwezi huu  linalojiita dola la Khorsan.

Soma:Taliban wauwa wapiganaji wawilli wa Dola la Kiislamu

Duru za kijasusi nchini Marekani zimethibitisha kwamba kiongozi wa kundi lenye mafungamano na IS ameuliwa. Mwishoni mwa juma lililopita jeshi la Marekani liliwajulisha wazazi wa wanamaji 11, baharia mmoja na askari waliouawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katikati ya umati wa Baba yake mmoja wa wanamaji waliofariki amesema taarifa ya kuuawa kwa muuaji wa mtoto wake imemletea faraja kidogo. Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani John Kirby amesema: "Marekani inajivunia kwamba iliweza kuwaondoa zaidi ya watu 124,000 kutoka Afghnistan lakini inahuzunika kwamba iliwapoteza maafisa weke. Amesema licha ya kupata mafanikio makubwa, lakini hiyo haimaanishi kuwa kila kitu kilienda vizuri katika zoezi hilo la kuwahamisha watu."

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani John Kirby.Picha: John Kirby/REUTERS

Maafisa wa Marekani wamesema nchi hiyo haikuhusika katika operesheni hiyo ya Taliban iliyosababisha kuuliwa mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga. Afisa mmoja wa utawala hata hivyo ameipongeza hatua hiyo muhimu ya Taliban.

Wanajeshi na wafanyakazi wengine waliouawa walikuwa miongoni mwa maafisa walioendesha uchuguzi wa usalama kwa maalfu ya Waafghanistan mnamo Agosti 26, mwaka 2021, waliojaribu kupata safari kwenye mojawapo ya ndege ili kuondoka nchini Afghanistan mara baada ya kundi la Taliban lilipochukua madaraka. Mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliushambulia umati wa watu kwenye uwanja wa ndege na baadae kundi linalojiita dola la kiislamu IS lilithibitisha kuhusika na shambulio hilo.

Soma:Guterres: Taliban iondoe zuio la wanawake kuajiriwa na UN

Kundi linalojiita dola la Khorsan lenye makao yake nchini Afghanistan na lenye uhusiano na IS lina wanachama wapatao 4,000 ni hasimu mkubwa wa kundi la Taliban na tishio kuu la kijeshi. Kundi hilo limeendelea kufanya mashambulio nchini Afghanistan tangu Taliban walipoingia madarakani.

Msemaji wa Taliban Bilal Karimi Picha: Bilal Guler/AA/picture alliance

Baada ya utawala wa Trump kufikia makubaliano na Taliban mnamo mwaka 2020 juu ya Marekani kuyaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan utawala wa Biden uliendelea na makubaliano hayo na hatimae zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Afghanistan lilifanyika mnamo mwaka 2021. Marekani ilitumaini kwamba hamu ya Wataliban ya kutambuliwa kimataifa na kupata msaada kwa ajili ya watu wa Afghanistan huenda ingewafanya kulegeza misimamo yao mikali.

Soma:Afghanistan: Wanawake waandamana kupinga marufuku dhidi yao

Uhusiano kati ya Marekani na kundi la Taliban umezidi kuzorota baada ya Taliban kuweka hatua mpya kali za kupiga marufuku wasichana kwenda shule na kuwakataza wanawake kufanya kazi kwenye mashirika ya misaada ya kimataifa na kwenye mashirika ya afya.

Vyanzo: AFP/AP/DPA