1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban wauwa wapiganaji wawilli wa Dola la Kiislamu

10 Aprili 2023

Wapiganaji wawili wa kundi lijiitalo Dola la Kiislamu wameuwawa katika operesheni huko katika mkoa wa kusini magharibi wa Nimruz nchini Afghanistan.

Afghanistan Kabul | Taliban Kämpfer in der Stadt
Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Shirika la habari la TOLO limeripoti kwamba katika operesheni hiyo iliyoendeshwa na Taliban iliyokuwa na makabiliano makali ya risasi, walifanikiwa kumkamata mpiganaji mmoja wa kundi hilo.

Tangu kurejea madarakani mnamo 2021, Taliban wamekuwa wakiwaandama wapinzani wao, huku kundi la Dola la Kiislamu nalo likizidisha mashambulizi yake kote nchini huku likiwalenga jamii za kidini za wachache, wanachama wa Taliban na maeneo ambayo wanadiplomasia wa kigeni wanaishi.

Soma zaidi: Shambulizi ya kujitoa muhanga laua watu 6 Afghanistan

Afghanistan imezidi kutengwa na nchi za Magharibi kutokana na sera kali za Taliban dhidi ya wanawake, kutozingatia kwao haki za binaadamu na kukataa kuunda serikali shirikishi.