1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Taliban yakana kushambulia msafara wa ubalozi, Pakistan

23 Septemba 2024

Kundi la wanamgambo wa Taliban la nchini Pakistan limekanusha kufanya shambulio la bomu dhidi ya msafara wa polisi uliokuwa ukiwasindikiza mabalozi wa nchi kadhaa katika eneo tete la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

Pakistan |
Vikosi vya usalama vimekuwa macho nchini Pakistan kutokana na kuendelea kwa visa vya mashambulizi nchini humo.Picha: Muhammed Semih Ugurlu/AA/picture alliance

Kauli hiyo ya msemaji wa kundi linalofahamika kama "Tehreek-e-Taliban-Pakistan" imetolewa wakati mamlaka za Pakistan zikisema bado zinaendelea na uchunguzi ili kubaini ni nani aliyehusika na shambulio hilo ambalo lilisababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi.

Mabalozi kutoka mataifa Indonesia, Ureno, Kazakhstan, Bosnia, Zimbabwe, Rwanda, Turkmenistan, Vietnam, Iran, Urusi na Tajikistan walishambuliwa hapo jana katika eneo la Malam Jabba wakiwa safarini kwenda Swat Valley, eneo ambalo liliwahi kuwa ngome imara ya kundi la Taliban la Pakistan.

Eneo hilo ni mojawapo ya vituo viwili vya mapumziko nchini Pakistan vinavyopatikana katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa unaopakana na Afghanistan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW