1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban yaadhimisha miaka mitatu madarakani

Hawa Bihoga
15 Agosti 2024

Kiongozi Mkuu wa Taliban nchini Afganistan Hibatullah Akhundzada amesema sheria za Kiislamu nchini humo zitatekelezwa katika kipindi chote cha utawala wao. Amesema hayo katika maadhimisho ya miaka mitatu madarakani.

Afghanistan | Taliban |  Naibu Waziri Mkuu anaeshughulikia Uchumi  Mullah Abdul Ghani Baradar.
Naibu Waziri Mkuu anaeshughulikia Uchumi aliechaguliwa na Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar akikagua gwaride katika maadhimisho ya miaka mitatu tangu walipotwaa madaraka.Picha: Siddiqullah Alizai/AP/picture alliance

Katika sherehe za kusherehekea mwaka wao wa tatu tangu kuutwaa mji mkuu Kabul, zimefanyika katika kituo cha zamani cha anga cha Marekani iliotumika kusuka mipango ya kuwaondoa Taliban madarakani.

Hotuba za viongozi hazikubeba ahadi za kumaliza changamoto za wananchi na badala yake ziliilenga jumuiya ya kimataifa, kuwataka kutoingilia masuala yake ya ndani huku wakiweka msisitizo katika kuimarisha sheria zinazotumika kuliongoza taifa hilo.

ambalo linakabiliana na vikwazo vya kimatatifa kutokana na kutajwa kukiuka haki za binaadamu hasa wanawake na wasichana.

Hotuba ya kiongozi mkuu wa Taliban ambae ni nadra kuonekana hadharani Hibatullah Akhundzada ilichapishwa kwenye mtandao wa X na msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid ilisema wanalo jukumu la kufuata sheria za kiislamu katika kuongoza.

"Ndugu zangu! Jukumu letu ni kutumikia dini, kutawala kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, ni jukumu letu la maisha yote." Ilisema sehemu ya hotuba yake.

Aliongeza kwamba mfumo wa sheria za kiislamu zinazotekelezwa na Taliban unazidi kuimarika siku hadi siku na kwamba hawatatetereka katika hilo.

Soma pia:Afghanistan yataka kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi yake

Akhundzada anatawala kwa amri akiwa katika mji wa Kandahar, mahali palipozaliwa vuguvugu la Taliban na ametoa amri kadhaa zinazotekeleza maono makali ya kundi hilo tangu kuanguka kwa serikali inayoungwa mkono na mataifa ya kigeni na kuondolewa kwa vikosi vilivyoongozwa na Marekani mwaka 2021.

Serikali ya Taliban bado haijatambuliwa na taifa lingine lolote, kutokana na kuweka vikwazo dhidi ya wanawake, sera ambazo Umoja wa Mataifa umeziita "ubaguzi wa kijinsia".

Hotuba za Taliban hazijatoa ahadi ya kumaliza matatizo ya wananchi

Katika mji wa Bagram ambako sherehe za maadhimisho zimefanyika Wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Taliban, walipongeza mafanikio yaliofikiwa hadi sasa ikiwemo kuimarishwa na kutumika kwa sheria za kiislam na kuanzishwa kwa mfumo wa kijeshi ambao waliutaja unatoa "amani na usalama kwa nchini."

Waziri wa Mambo ya Ndani wa taliban Sirajuddin Haqqan akihudhuria sharehe za maadhimisho ya miaka mitatu tangu walipotwaa madaraka.Picha: Siddiqullah Alizai/AP/picture alliance

"Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Emirate iliridhia makubaliano ya Doha, hakuna mtu aliyedhuriwa na Afganistan na tunaahidi katika siku zijazo hakuna mtu ambaye atadhuriwa katika ardhi ya Afghanistan."  Alisema Naimu Waziri Mkuu alieteuliwa na Taliban Maulvi Abdul Kabir 

Hata hivyo hakuna wazungumzaji wengine ambao walizungumza kuhusu changamoto zinazowakabili Waafghanistan katika maisha ya kila siku.

Kwa miongo kadhaa machafuko na ukosefu wa utulivu umewaacha mamilioni ya raia wa taifa hilo kwenye ukingo hatari wa njaa, ukosefu mkubwa wa ajira kadhalika uminywaji wa haki za binaadamu hasa wanawake.

Soma pia:Wasichana milioni 1.4 wazuiwa kwenda shule za sekondari nchini Afghanistan

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Wanawake nchini Afghanistan, Alison Davidian amesema wanawake wameendelea kushuhudia mbinyo katika haki na hata wale waliojaribu kushiriki katika muundo wa serikali walitumika kufuatilia ufuasi wa wanawake wengine katika kutekeleza kanuni za Taliban za kibaguzi.

Ama kwa upande wake Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock kupitia maadhimisho haya ameonesha namna ambavyo makundi ya wasichana na wanawake nchini humo yanavyoendelea kupokwa haki ya kuishi maisha yao ya kawaida.

 "Nusu ya nchi hairuhusiwi tena kufanya kile ambacho ni sehemu ya maisha ya kawaida: kazi, kwenda hospitalini peke yako, kuonyesha nyuso zao hadharani, kwenda shuleni wakiwa vijana, badala yake kuwa mwanamke,"

Uchambuzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2026, athari za kusababisha wasichana milioni 1.1 kukosa shule na wanawake 100,000 kutokuwa vyuo vikuu zinahusiana na ongezeko la uzazi kwa asilimia 45 na ongezeko la vifo vya uzazi kwa hadi asilimia 50.

Wanawake wa Afghanistan waelezea maisha yao kupitia uchoraji

02:56

This browser does not support the video element.