1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Taliban yahudhuria kikao kinachongozwa na Umoja Mataifa

30 Juni 2024

Wajumbe wa kundi la Taliban wamehudhuria mkutano unaongozwa na Umoja wa Mataifa nchini Qatar baada ya waandaaji kusema wanawake hawatajumuishwa.

Qatar | Ujumbe wa Taliban
Wajumbe wa kundi la Taliban wakiwa mjini Doha kwa mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa.Picha: Zabihullah Mujahid

Mkutano huo wa siku mbili ni watatu ili kujadili mzozo wa Afghanistan.

Soma pia: Taliban: Haki za wanawake wa Afghanistan ni suala la ndani

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, msemaji mkuu wa serikali ya Taliban, Zabihullah Mujahid, ambaye anaongoza ujumbe huo amesema wamekutana na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Urusi, India na Uzbekistan.

Taliban hawakualikwa kwenye mkutano wa kwanza, ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema masharti ya kuhudhuria kwao walitaka wanachama wa jumuiya ya kiraia wa Afghanistan kutengwa katika mazungumzo hayo na kwamba Taliban wachukuliwe kama watawala halali wa Afghanistan.

Hata hivyo, kufikia sasa hakuna nchi ambayo imeutambua rasmi utawala wa Taliban nchini Afghanistan, na Umoja wa Mataifa umesema itakuwa vigumu kutambuliwa kwa utawala huo, hasa kutokana na kuendeleza marufuku ya elimu na ajira kwa wanawake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW