Taliban yakanusha madai ya Pakistan kushambulizi mipakani
12 Septemba 2023Pakistan iliufunga mpaka wa Torkham upande wa kaskazini magharibi Jumatano iliyopita baada ya walinzi wa nchi hizo mbili kushambuliana kwa risasi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Pakistan Mumtaz Zahra Baloch ameushtumu utawala wa Talibankwa kujenga majengo haramu kwenye maeneo ya mipaka na kufanya mashambulizi ya risasi kama uchokozi.
Soma pia:Taliban yasaini makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 6.5 nchini Afghanistan
Baloch amerudia madai kwamba Afghanistan inaruhusu ardhi yake kutumika na wanamgambo kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan.
Matamshi ya Baloch yameukasirisha utawala wa Taliban, huku afisa mmoja wa Taliban akiitaja serikali ya Pakistan kama "isiyokuwa na uwezo" na kwamba haiwezi kuhakikisha usalama wa taifa.
Nchi hizo mbili, Afghanistan na Pakistan, zimekuwa zikilaumiana kwa muda mrefu juu ya mzozo kwenye mipaka yao na suala la usalama.