1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Taliban yaridhia kuongezwa muda wa ujumbe wa UNAMA

16 Machi 2024

Utawala wa Taliban umekaribisha uamuzi wa kuongezwa muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Deborah Lyons
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Deborah Lyons Picha: Ajjad Hussain/AFP/Getty Images

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ameliambia shirika la habari la serikali RTA kuwa, kuongezwa kwa muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNAMA kutasaidia kuimarisha maslahi ya Afghanistan hasa wakati huu ambapo nchi hiyo inajaribu kuimarisha uhusiano wake na mataifa mengine.

Mujahid ameitolea mwito UNAMA kuielezea jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua za maendeleo ilizopiga nchi hiyo huku akilaani "ukosoaji usiokuwa wa haki" kwa Afghanistan.

Soma pia: Umoja wa Mataifa waahidi kubakia Afghanistan 

Msemaji huyo pia amehimiza kuachiliwa kwa akiba ya fedha za kigeni ya nchi hiyo.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umekuwepo nchini humo tangu mwaka 2022 na sasa muda wake wa kuhudumu umeongezwa hadi Machi 17, 2025 kwa kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iliyofanyika jana.

Serikali ya Taliban haijatambuliwa rasmi na nchi yoyote tangu ilipoingia madarakani baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani Agosti mwaka 2021 huku kukiwa na wasiwasi juu ya haki za wanawake na kudorora kwa usalama.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW