1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban yamzuia mtaalamu wa UN kuingia Afghanistan

22 Agosti 2024

Serikali ya Taliban imemzuia mtalaamu aliyeteuliwa na Umoja wa Mataifa Richard Bennett kuingia nchini Afghanistan kwa kuishutumu taasisi ya haki za binaadamu ya umoja huo kwa kueneza propaganda.

 Umoja wa Mataifa | Richard Bennett
Mtalaamu wa Umoja wa Mataifa Richard Bennett Picha: Jean Marc Ferré/MAXPPP/picture alliance

Bennett aliteuliwa na Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa mwaka wa 2022 kufuatilia hali ya haki za binaadamu nchini Afghanistan baada ya Taliban kuchukua usukani mwaka uliotangulia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya serikali ya Taliban Abdul Qahar Balkhi amesema Bennett ameshindwa kupata viza ya kuingia Afghanistan. 

Bennett, ambaye hapo awali alisema vitendo vya Taliban dhidi ya wanawake na wasichana vinaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu, anahudumu nje ya Afghanistan lakini ameitembelea nchi hiyo mara kadhaa kutafiti hali ya haki za binaadamu.

Soma pia:Wasichana milioni 1.4 wazuiwa kwenda shule za sekondari nchini Afghanistan

Mjumbe huyo amesema katika taarifa kuwa anayachukulia majukumu yake kwa umuhimu mkubwa.

Ameihimiza Taliban kuubatilisha uamuzi wake na kusema kuwa ataendelea kushirikiana na Waafghanistan ndani na nje ya nchi hiyo. Miaka mitatu baada ya kuingia madarakani kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni, Taliban haijatambuliwa rasmi na serikali yoyote ya kigeni. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW