1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tangazo la vizuizi bandari za Iran lapandisha bei za mafuta

13 Aprili 2026

Bei za mafuta zimepanda katika mnada wa awali wa masoko ya Marekani baada ya Washington kutangaza vizuizi kwa bandari zote za Iran pamoja na meli za mafuta zitakazopakia shehena kutoka nchini humo.

Meli za mafuta
Meli za mafuta.Picha: Altaf Qadri/AP Photo/picture alliance

Gharama ya pipa moja la mafuta ghafi ya Marekani imepanda kwa asilimia 8 na kufikia dola 104 huku katika soko la dunia pipa moja la mafuta linauzwa kwa dola 102 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.

Bei ya mafuta imeyumba mara kadhaa wakati wa vita vya Iran, ikipanda kutoka dola 70 kwa pipa kabla ya vita na kufikia hadi karibu dola 120.

Kabla ya kuanza mazungumzo kati ya Iran na Marekani nchini Pakistan, bei ya mafuta ilishuka kidogo kwenye soko la dunia kwa matumaini mwafaka ungepatikana na kuondoa vizuizi hasa kwenye Mlango Bahari wa Hormuz ambao sasa unadhibitiwa na Tehran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW