1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania, EU kutanua wigo wa biashara

23 Februari 2023

Umoja wa Ulaya na Tanzania leo zimekubaliana kupanua wigo zaidi wa biashara hasa wakati huu ambako taifa hilo la Afrika Mashariki likianza kujifungua upya katika mashirikiano ya kimataifa.

Tansania Eisenbahnbau
Picha: ERICKY BONIPHACE/AFP

Pande hizo mbili zimefungua jukwaa la kibiashara ambalo limewaleta pamoja zaidi ya wawekezaji na wafanyabiashara 700 wanaokutana kwa siku mbili katika jiji la kibiashara la Dar es salaam.

Kwa kiasi gani pande hizo mbili yaani nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na Tanzania zinavyoweza kuzitumia fursa zinazopatikana na kuzigeuza tuna ya ukuzaji biashara ndiyo sehemu kubwa ya majadiliano yanayoendelea wakati wafanyabiashara na wawekezai walivyoanza siku ya kwanza ya kongamano hilo.

Maeneo yanayohusu sekta ya kilimo, utalii, nishati ya umeme pamoja na uzalishaji jumla wa malighafi yanaonekana pia kuangaziwa zaidi na pande zote mbili hasa wakati ambako serikali ya Tanzania ikichukua mkondo mpya wa kisera wenye lengo la kuwaletea uhakika wa uwekezaji wafanyabiashara wa kimagharibi.

Makamu wa Rais wa Tanznaia, Dr Philip Mpango aliyefungua kongamano hilo metumia sehemu kubwa ya hotuba yake kuwapa picha kuelezea mweleko mpya inaochukuliwa na serikali akisema taifa hikli sasa limezaliwa upya na kwa maana hiyo wawekezaji wa kigeni wanakariishwa mikono miwili kuleta vitego uchumi vyao.

Amesema,Tanzania itaendelea kuwa mshirika mwema wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na inawakaribisha wawekezaji wa binafsi kuja kushirikiana na wale wa Tanzania ili biashara ya pande hizo mbili ipate msukumo mpya na kunawili zaidi.

Tangu kuanzishwa kwa mashirikiano na Umoja wa Ulaya katika kipindi cha miaka 1970, Tanzania imefaidika ufadhili wa miradi ya aina mbalimbali inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3. Nayo Benki ya uwekezaji ya Umoja wa Ulaya yenye makao yake Luxembourg imeahidi kurejea tena nchini baada ya kutoweka miaka saba iliyopita.

Imelenga kupiga jeki miradi yanayohusu nishati yadidifu, uwekezaji katika sekta ya maji  huku ikitarajia kutenga kiasi chaa euro milioni 540 kitakachotumika kama uwekezaji mpya kwa wafanyibiashara wa Kitanzania.

Waziri wa uwekezaji, biashara na viwanda Dr Ashata Kijatu amesema, jukwaa hili la kibiashara ni hatua inayotoa mwongozo wa namna biashara zinavyoweza kunufaisha pande zote mbili.

Kongamano hilo ambalo pia linahuduhuria na wanadiplomasia wa pande zote mbili linatarajiwa kufungwa hapo kesho na Rais wa Zanzibar, Dr Hussen Ally Mwinyi.

George Njogopa, DW Dar es Salaam

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW