Tanzania inaweza kujifunza nini kutoka kwa Kenya?
21 Oktoba 2015Matangazo
Wakati hali ikionekana kuwa shwari kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba, kuna wasiwasi pia unaojitokeza wa kutokuwepo hali nzuri ya usalama nchini Tanzania wakati wa mchakato wa kupia kura na pengine hata baadaye. Wasiwasi huo unatokana na sababu mbali mbali zinazotajwa na wadadisi wa mambo wanaofuatilia uchaguzi huo.
Mwaka 2007 Kenya ilitumbukia katika ghasia kubwa zilizosababisha umwagikaji mkubwa wa damu ambao hauwezi kusahaulika katika historia ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Je, matukio ya Kenya yametoa somo gani kwa wananchi wa Tanzania wanaosubiri kupiga kura?
Saumu Mwasimba amejadili suala hilo na Richard Shaba, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na Mratibu Mipango wa wakfu wa Kijerumani wa Konrad Adenauer nchini Tanzania.