Tanzania kuendelea kushirikiana na mashirika ya kiraia
30 Septemba 2021Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ameitoa hii leo wakati akihutubia mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Tanzania, mkutano uliofanyika katika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu- "Kuimarisha mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika maendeleo ya taifa"
Rais Samia amesema kuwa mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika harakati za kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Daktari Lilian Badi, amesema kuwa mashirika hayo nchini Tanzania yamekuwa yakikabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinakwamisha utendaji wake.
Mkutano huu wa mwaka wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Tanzania umefanyika huku kukielezwa kuwepo na uminywaji wa uhuru wa mashirika hayo ikiwemo baadhi kufungiwa kufanya shughuli zake nchini humo.