1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kuikabili Nigeria kwenye AFCON mechi yao ya kwanza

23 Desemba 2025

Mechi ya mapema kabisa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dhidi ya Benin majira ya saba na nusu kwa majira ya Morocco. Baadaye jioni,Tanzania itamenyana na Nigeria kwa mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu kwa Stars.

Tanzania - Kongo
Timu za Tanzania, Kongo na Uganda kuanza safari yao ya AFCON 2025 hii leo nchini MoroccoPicha: Fadel SennaAFP/Getty Images

Michuano ya kandanda kwa mataifa ya Afrika -AFCON 2025 - inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi leo hii nchini Morocco kwa mechi kadhaa. Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwenye michuano hiyo wanatupa karata zao za kwanza uwanjani leo Jumanne.

Mechi ya mapema kabisa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dhidi ya Benin majira ya saba na nusu kwa majira ya Morocco. Baadaye jioni, Taifa Stars ya Tanzania itamenyana na Nigeria kwa mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu kwa Stars ambayo imekuwa na historia isiyoridhisha kwenye michuano hiyo. 

Mechi ya usiku wa leo itakuwa kati ya Uganda na Tunisia. 

Hapo jana, Mali iliyo kundi A ililazimishwa sare ya1-1kwenye mchezo wake na Zambia. Bafana Bafana ya Afrika Kusini iliondoka na alama tatu kwa kuichapa Angola mabao 2-1. Matokeo sawa na hayo yalipatikana pia na Mafarao wa Misri walioilaza Zimbabwe bao 2-1.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW