1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Kupekua simu ya mwenzi wako faini hadi ml.20

4 Novemba 2024

Kumekuwa na mseto wa mawazo nchini Tanzania, baada ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Ludewa, Tanzania, Celestine Luhende kusema, mwanandoa kupekua simu ya mwenza wake atapigwa faini hadi Tsh milioni 10 pamoja na kifungo.

Teknolojia I Haki za Binadamu | Mawasiliano
Mtu akipekuwa simu ya mkononiPicha: Peter Byrne/empics/picture alliance

Akizungumza katika kikao cha madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Ludewa, jana Kamanda huyo wa Polisi amesema, ukipatikana na hatia ya kupekua simu ya mwenza wako, adhabu yake ni kuanzia Tsh milioni tano hadi milioni 20.

"Ukipatikana na hatia kwa kupekuwa simu ya mwenza wako, adhabu yake ni tsh. milioni 5 hadi milioni 20" Alisema mkuu huyo wa polisi wilaya.

Hata hivyo hoja hii ya OCD Luhende, imetafsiriwa kwa mitazamo tofauti na wanasheria, wanasaikolojia na wanandoa hapa nchini.

 Wanasheria, waliozungumza na DW Kiswahili wameeleza kuwa hakuna sheria inayosema moja kwa moja kuwa ni kosa kisheria kupekua simu ya mwenza, badala yake walifafanua na kusema kuwa ipo sheria inayokataza kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine.

Soma pia:Meta kuchunguzwa juu ya usalama wa watoto mtandaoni

 Wakili Paul Kisabo, amezungumza na DW na kufafanua kuhusu sheria hiyo, akisema hakuana sheria inayozungumzia hilo ispokuwa katiba imefafanua juu katiba kuhusu haki ya faragha. 

"Kwa mujibu wa katiba, ibara ya 16 inatoa haki ya faragha, haki ya faragha ni pamoja na kuingilia mawasiliano yake"

Tanzania: Ni kosa kutokuweka "password" kwenye simu yako

Kwa upande wake, Mwanasheria aliyejikita katika masuala ya usalama wa mawasiliano, (Cyber-security) Fulgence Masawe, amesema kisheria ni kosa kutokuweka nywila kwenye simu yako na sheria haisemi iwapo kosa hilo lina adhabu.

Vigezo vya kuzingatia unapoomba au unapokubali urafiki mitandaoni

03:11

This browser does not support the video element.

Pamoja na Wanasheria, wanandoa nao walikuwa na haya ya kusema kuhusu utata wa sheria hiyo.

 Shadida Dalanga, mkazi wa Tunduma, Tanzania amesema si sawa kutoza faini ya kiasi hicho cha fedha sababu ni faranga za watu wawili walio kwenye mahusiano.

"Ingawa tunafahamu kuwa si jambo zuri, lakini sidhani kama adhabu inafaa kuwa milioni 5, sababu ni kuingilia jambo la ndani kati ya watu wawili."

Soma pia:Mtaalamu wa mitandao wa Marekani afungwa jela miaka 21

John  Ambrose,  Mkazi wa Dar es Salaam kwa upande wake ameona sheria hiyo inafaa katika kulinda maslahi ya mahusiano baina ya mke na mume "lengo kulinda maslahi ya watu wawili na ustawi wa jamii kwa ujumla wake."

Mwanasaikolojia wa masuala ya mahusiano Chris Mauki amesema yapo makubaliano kwa wanandoa kuhusu matumizi ya simu za mkononi ambayo ni vigumu kusimamia na sheria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW