1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kutumia trilioni 41 katika mwaka wa fedha 2022/23

Deo Kaji Makomba
14 Juni 2022

Serikali ya Tanzania imewasilisha bungeni bajeti yake kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo jumla ya shilingi trilioni 41.48 zinatarajiwa kutumika. Shilingi trilioni 28.02, zitatokana na vyanzo vya ndani.

MWIGULU NCHEMBA
Picha: Deo kaji Makomba/DW

Akisoma bajeti kuu hiyo hii siku ya Jumanne bungeni jijini Dodoma, waziri wa Fedha na mipango Mwigulu Nchemba amesema misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 4.65, sawa na asilimia 11.2 ya bajeti yote, huku Serikali ikitarajia kukopa shilingi trilioni 5.78 kutoka soko la ndani ambapo shilingi trilioni 3.30 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na kiasi cha shilingi trilioni 2.48 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo huku akigusia sekta ya kilimo.Jumuiya ya Afrika Mashariki yapitisha bajeti yake

Kati ya mapato hayo, kiasi kitakachokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 23.65 na mapato yasiyo ya kodi kutoka wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 4.37.

Biashara maarufu ya mitumba KariakooPicha: Said Khamis/DW

Aidha waziri Nchemba ameongeza kuwa bajeti ya mwaka 2022/23 inalenga kuongeza kasi ya kufufua uchumi na kuimarisha sekta za uzalishaji kwa ajili ya kuboresha maisha, hivyo nguvu kubwa itaelekezwa katika maeneo hayo chini ya kaulimbiu ya Kazi Iendelee na pia suala la elimu bure litakuwa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

Bajeti kuu Kenya yagonga sh. 3.3 TrilionAwali akisoma taarifa ya hali ya uchumi ya taifa, waziri Mwigulu amesema kufikia Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa Sh69.44 trilioni ikilinganishwa na Sh60.72 trilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.4. Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Sh47.07 trilioni na deni la ndani lilikuwa Sh22.37 trilioni.