1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania inaadhimisha miaka 26 ya kifo cha Nyerere

14 Oktoba 2025

Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa Julias Nyerere huku ikiwa katika hatua za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu uliowagawa wananchi kisiasa baada ya chama kimoja cha upinzani kususia uchaguzi huo.

ulius Nyerere
Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Picha: AFP/Getty Images

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere leo (14.10.2025) anatimiza miaka 26 tangu afariki dunia na anakumbukwa wakati taifa likiwa katika heka heka ya kuelekea uchaguzi mkuu. Nyerere ambaye anatajwa kuwa mpania demokrasia ya kweli, ndiye aliyeweka ushawishi kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi ambavyo baadhi yake leo vinajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa hapo Oktoba 29.

Ingawa uchaguzi huu umesusiwa na chama kikuu cha upinzani Chadema kwa madai ya kufanyika kwa kwanza mageuzi katika mifumo ya uchaguzi,  unashuhudiwa vyama vikiendelea kuzunguka kwa wapiga kura kwa ajili ya kunadi sera zao.

Hata hivyo, chama tawala CCM ndicho kinachoonekana kuyatawala zaidi majukwaa ya kampeni na imechangiwa zaidi ni misuli yake ya kiuchumi wakati wagombea wengine wakilalamika kukabiliwa na uhaba wa fedha.

Baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wanaona kwamba uchaguzi wa mwaka huu huenda ukawa mtihani mwingine wa demokrasia ya Tanzania kutokana na kususia na ngome ya upinzani. Hata hivyo, mfuatiliaji wa mambo Bashir Hoza anasema kiu ya wananchi katika uchaguzi huu ni kuona namna wagombea watakavyoshughulikia kero zao iwapo watapatiwa ridhaa ya kuingia kwenye uongozi.

Wagombea hawana imani na ahadi za viongozi wao

Ama kwa upande mwingine baadhi ya wapiga kura wanasema wanapoadhimisha kifo cha Baba wa Taifa wakati huu ambako taifa linaelekea katika uchaguzi bado wamevunjika moyo na ahadi zisizotekelezeka kutoka kwa wagombea. Wanaamini kuwa baadhi ya wagombea hao hutembea na ajenda za siri moyoni, huku wakishindwa kuyasimamia yale ambayo Baba wa Taifa aliyapigania.

Hivi sasa wagombea kuanzia ngazi ya urais, ubunge mpaka udiwani wako katika kipindi cha lalasama cha kampeni kabla ya kuacha ukumbi kwa wapiga kura kuamua hapo Oktoba 25.

Na kiasi gani wapiga kura wataremka katika vituo vya wapiiga kura bado ni swali linalosubiriwa kuteguliwa siku ya upigaji kutokana na baadhi yao kugawika kama hatua ya kuunga mkono uamuzi uliochukuliwa na chama kikuu cha upinzaniCHADEMAkujiweka kando na uchaguzi huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW