Tanzania: Mvutano wazuka juu ya hati ya Muungano
4 Aprili 2014Matangazo
Suala la kugushiwa kwa saini ya mmoja kati ya waasisi wa muungano hayati, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar limekuwa kama kikwazo kingine katika maendeleo ya mijadala ya bunge la katiba. Sudi Mnette amezungumza na Richard Shaba kutoka wakfu wa Konrad Adenauer nchini Tanzania.Kwanza alitaka kujua hali ya kutoonekana hasa kwa hati halisi ya muungano kama invyohitajika katika bunge la katiba anaizungumziaje?
Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za maskioni hapo chini.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdulrahman