1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania - Burundi zawasihi wakimbizi kurejea kwao

Prosper Kwigize6 Agosti 2024

Manaibu waziri wa mambo ya ndani wa Burundi na Tanzania wametembelea kambi ya wakimbizi Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kwa lengo la kuwahamasisha wakimbizi wa Burundi kurejea nyumbani baada ya zoezi hilo kusua.

Wakimbizi wakiwa kwenye kambi
Wakimbizi wakiwa kwenye kambiPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Serikali za Tanzania na Burundi kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi zimekuwa katika mpango mahususi wa kuwashawishi wakimbizi wa Burundi kurejea nchini mwao huku kukiwepo na mkakati wa kufunga kambi zinazowahifadhi mkoani Kigoma nchini Tanzania.

Malengo hayo yamewaleta Pamoja viongozi wa serikali hizo wakiwakilishwa na Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Daniel Sillo na Naibu Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi brigedia jenerali Nimbona Bonansize ambao wamezuru katika kambi ya wakimbizi ya nyarugusu kuwashawishi wakimbizi hao kurejea

Akizungumza na wakimbizi hao Naibu Waziri wa Nambo ya Ndani wa Tanzania Daniel Sillo amesema Tanzania inatambua hali ya amani na utulivu iliyopo Burundi na ndio maana inashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kurejesha wakimbizi

Kwa upande wake Naibu Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi ambaye amefuatana na raia kadhaa waliowahi kuwa wakimbizi na kuamua kurejea nchini mwao amebainisha kuwa nchi hiyo imeweka mazingira mazuri ili kupokea na kutoa huduma kwa wakimbizi wanaorejea ikiwa ni Pamoja na kuwahakikishia usalama

Tanzania: Wakimbizi wanapaswa kurejea nyumbani

Kwa upande wake mratibu wa idara ya wakimbizi wa serikali ya Tanzania Bw. Sudi Mwakibasi amebainisha kuwa Tanzania inaridhika kuwa wakimbizi waliopo Tanzania wanao wajibu wa kurejea nchini mwao kwakuta taarifa za kutosha kuhusu amani na usalama wao wanaporejea zimeshasambazwa na zinajitosheleza

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na Uingereza ziarani Kigoma

04:15

This browser does not support the video element.

Mkuu wa ofisi ya UNHCR Kasulu Jean Bosco ambaye ni mwenyeji wa mpango wa kuja kushuhudia na kushawishi wakimbizi kurejea, amesema UN itaendelea kutoa huduma wezeshi ili wakimbizi walioko tayari kurejea warejee kwa amani na utu

Kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma ina jumla ya wakimbizi 134,920 Ikiwa ni wakongo 87190 na Warundi ni 47888 huku watu 1658 ndio walio jitolea kurejea kwa hiari nchini burundi kwa mwaka 2024 ambapo ni nje ya malengo ya 38,000  sawa na watu 2000 kila wiki na lengo hili halijawah kufikiwa

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW