1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege mbili zaanguka Hifadhi ya Mikumi Tanzania

30 Novemba 2023

Ndege mbili za abiria zilizokuwa zimebeba watalii zimeanguka siku moja katika uwanja wa Kikoboga katika mbuga ya wanyama ya Tanzania lakini maafisa wamesema watu wote waliokuwemo ndani ya ndege hizo wamenusurika.

Emiliano Sala bei Flugzeugabsturz verunglückt
TANAPA imesema abiria wote waliokuwa kwenye ndege zilizoanguka walinusrika.Picha: AAIB/PA Wire/empics/picture alliance

Ndege mbili za abiria zilizokuwa zimebeba watalii zimeanguka siku moja katika uwanja wa Kikoboga katika mbuga ya wanyama ya Tanzania, lakini maafisa wamesema watu wote waliokuwemo ndani ya ndege hizo kutoka na kuelekea Zanzibar wamenusurika bila kujeruhiwa.

Mamlaka ya hifadhi nchini Tanzania (TANAPA) imesema matukio yote mawili yalihusisha ndege zinazomilikiwa na shirika la ndege la Unity Air, na yalitokea siku ya Jumanne katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi inayopatikana mashariki mwa nchi hiyo. Jumla ya abiria 60, pamoja na wahudumu saba walikuwa kwenye safari hizo.

TANAPA imesema hadi sasa chanzo cha ajali hizo hakijafahamika. Novemba mwaka jana, watu 19 walikufa baada ya ndege ya shirika la Precision Air kuanguka katika Ziwa Victoria, ikiwa ni ajali mbaya zaidi ya anga kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa nchini Tanzania.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW