1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Tanzania yazindua rasmi safari za treni ya SGR

1 Agosti 2024

Historia imeandikwa nchini Tanzania baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi safari za treni ya umeme wa SGR utakaofanya safari zake kati ya Dodoma na Dar es Salaam.

Rais wa Tanzania Samia Suhulu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi safari za treni ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi DodomaPicha: Florence Majani/DW

Historia imeandikwa. Hivyo ndivyo tunavyoweza kusema, baada ya usafiri wa treni za kisasa zinazotumia umeme (SGR) na zinazokwenda kwa kasi kuzinduliwa rasmi leo, na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Leo Agosti Mosi, Rais Samia, amezindua rasmi usafiri wa treni hizo kwa kutumia treni inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma.

Soma pia: Watanzania waanza kufurahia usafiri wa treni ya kisasa inayotumia umeme (SGR)

Saa 5 na nusu asubuhi, Rais, Samia, alipanda treni hiyo na kuketi katika behewa la hadhi ya juu (presidential suits) tayari kwa kuanza safari kuelekea Dodoma, ikiwa ni ishara ya uzinduzi kamilifu.

Mradi wa treni ya umeme Tanzania uligharibu kiasi cha shilingi trilioni 10 kutoka Dar es Salaam hadi DodomaPicha: Ericky Boniphace/AFP

Treni ya kisasa iliyozinduliwa Alhamisi, imegharimu kiasi cha TSh 10 trilioni, na inatarajiwa kutembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa, hiyo ikimaanisha wasafiri watatumia takribani saa 2 kutoka Dar  es Salaam Kwenda Dodoma.

 Treni hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba tani 10 elfu za mizigo, sawa na malori 500 ya mizigo, na zinatarajiwa kuiunganisha Tanzania na nchi zisizopakana na Bahari ikiwamo Burundi, Congo na Rwanda. Kadhalika, mradi wa treni hizo unatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya  elfu 15 kwa wazawa.

Soma pia: Tanzania yasaini mkataba wa reli wa dola bilioni 2.2 na China

Leo ni ishara ya mwendelezo wa uzinduzi huu ambapo Julai mwaka huu, treni ya safari za treni hizo kati ya Dar es Salaam na Morogoro zilizinduliwa.

Akizungumza mara baada ya kuanza safari hiyo, Rais Samia amesema, nia ya kuunganisha usafiri huo wa kisasa na DRC na Burundi ni masoko.

Uzinduzi wa treni hiyo ya kisasa, ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wakiwamo wakuu wa Wilaya, wakuu wa Mikoa, viongozi wastaafu,  rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, viongozi wa kisiasa na wanahabari.