Tanzania: Suala la Zanzibar ni nchi au si nchi
9 Julai 2008Matangazo
Sintofahamu hiyo ilikuja baada ya waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kusema ya kwamba Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya muungano.
Kauli yake hiyo ilizusha mjadala mkali katika baraza la wawakilishi huko Zanzibar ambapo mwanasheria mkuu wa wa huko Pandu Amir Kificho alitoa ufafanuzi kuwa Zanzibar ni nchi na kwamba Waziri Mkuu wa muungano aliteleza.
Aboubakary Liongo amewasiliana na Waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na masuala ya muungano Bw. Mohamed Seif Khatib ili kupata ufafanuzi juu ya suala hilo.