1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania, Uganda zaanza vibaya AFCON

24 Desemba 2025

Tanzania na Uganda zimeanza vibaya michuano ya kandanda kwa mataifa ya Afrika- AFCON 2025 kwa kukubali kichapo kwenye mechi zao za ufunguzi zilizichezwa jana.

Afrika-Cup 2025 | Mchezo kati ya Uganda na Tunisia
Mchezo kati ya Uganda na Tunisia. Picha: Sebastien Bozon/AFP

Taifa ya Stars ya Tanzania ilishindwa kutamba mbele ya Nigeria na kukubali kichapo cha shingo upande cha magoli 2-1.

Uganda The Cranes wenyewe walijikuta kwenye hali mbaya zaidi kwa kubamizwa goli 3-1 walipokwaana na Tunisia mjini Rabat.

Hata hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imewapa matumaini ya awali mashabiki wa soka wa Afrika Mashariki na Kati kwa ushindi wa kupapatua wa bao 1-0 mbele ya Benin.

Kwenye mechi nyingine, timu ya taifa ya Senegal au Simba wa Teranga, walikunjua makucha na kuwararua bao 3-0 vijana wa Botswana.

Hii leo mechi za ufunguzi wa hatua ya makundi zinamalizika kwa michezo minne ikiwemo itayaowakutanisha Ivory Coast dhidi ya Msumbiji na Algeria itakuwa na miadi na Sudan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW