Tanzania, Uganda zakubaliana kuimarisha biashara, uwekezaji
10 Mei 2022Hatua ya kuondoa vizingiti hivyo maarufu kama NTBs inafuatia majadiliano kati ya maafisa wa ngazi za juu kutoka Tanzania na Uganda waliokutana mwezi Januari mwaka huu.
Marais hao wawili wameagiza kwamba maafisa watendaji wawe wakikutana kila mwezi kuona kwamba vizingiti vyovyote vinavyojitokeza vinashughulikiwa ili kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili na pia Afrika Mashariki.
Miongoni mwa kero kubwa kwa wafanyabiashara nchini Uganda na katika mataifa ya Afrika Mashariki imekuwa ada inayotozwa magari ya mizigo hii ikiwa dola 520 kwa kila gari ya kigeni inayopitia barabara za Tanzania.
Lakini sasa magari yatakuwa yakitozwa dola kumi tu kwa kila kilomita mia moja ikimaanisha kuwa kati ya Mutukula na Dar Es Salam umbali wa kilomita 1,500 za barabara yatalipa dola 150 za Kimarekani.
Pande zote aidha zimekubaliana kuruhusu shehena ya sukari ya tani 10,000 kuuzwa Tanzania ili kuziba upungufu wa bidhaa hiyo nchini humo.
Wakati huohuo, Uganda itasambaza nyaya ya umeme kuweza kukidhi mahitaji katika mikoa ya hadi Mwanza. Pia Tanzania itagiza bidhaa za matibabu zinazotengenezwa Uganda.
Taarifa ya mkurugezi wa mawasiliano ya ofisi ya rais wa Tanzania, ilisema madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kudumisha zaidi historia iliyopo na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa hiyo iliitaja ziara hiyo kuwa ya kwanza ya kiserikali kufanywa na Rais Samia tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwezi Machi 2021.