1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya Uhuru

George Njogopa9 Desemba 2021

Tanzania leo imehitimisha kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa iliyokuwa Tanganganyika katika sherehe za kusimumua zilizohuhudhuriwa pia na viongozi mbalimbali kutoka Afrika.

Julius Nyerere erster Präsident Tansania
Picha: Getty Images/AFP

Gwaride la kijeshi pamoja na maonyesho ya halaiki ni baadhi ya mambo yaliyooamba maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Ni sherehe zilitawaliwa na kila aina ya hamasa huku umati mkubwa wa wananchi wakifika katika uwanja wa uhuru, wakivutiwa matukio ya aina mbalimbali yaliyoanza kushuhudiwa tangu saa mbili asubuhi na kuendelea hadi nyakati za saa nane mchana.

Soma zaidi: Serikali ya sasa ya Tanzania kwenda kinyume na iliyopita

Waziri Mkuu Kassim Majiliwa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo, alisema kwa namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi ni ushuhuda tosha kwamba taifa hili limesafiiri miaka 60 ya uhuru katika njia ya amani na utulivu.

Rais Samia aliyeongoza maadhimisho haya, ikiwa ni ya kwanza katika utawala wake, alikuwa ameungwa mkono na marais wengine kutoka ukanda wa Afrika, ikiwamo Msumbiji, Rwanda, Comoro na Kenya ambayo Rais wake Uhuru Kenyatta kama alivyosema Rais Samia mwenyewe ataendelea kusalia nchini kwa siku.

Rais Samia kwenye maadhimisho hayo hakuwa na hotuba ndefu mbali ya kuwatambulisha wageni wake lakini alitumia muda mwingi kwenye hotuba aliyotoa hapo jana usiku kutaja mafanikio yaliyofikiwa tangu taifa hili lilipopeperusha kwa mara ya kwanza bendera yake mnamo Disemba 9, 1961.

Soma zaidi: Asasi za kiraia Tanzania zapinga kauli kutumiwa na wadhamini

Kama sehemu ya maadhimisho hayo kuna uwezekano Rais Samia akatumia desturi ya watangulizi wake kutangaza msamaha kwa wafunguwa walioko gerezani ingawa haijafahamika kama hilo litafanyika ni wafungwa wa aina gani watakaonufaika na msamaha huo na idadi yao itakuwaje.

Wakati wote tangu kuanza kwa shamra shmra za maadhimisho hayo, kumekuwa kukifanyika makongamano na mijadala inayojaribu kutathmini hali ya nchi baada ya uhuru wa miaka 60 na hali jumla ya baadaye.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW