Tanzania yaanzisha operesheni dhidi ya ongezeko la mauaji
27 Januari 2022Sehemu kubwa ya mauwaji hayo yanahusisha mahusiano ya kimapenzi na tamaa ya kutaka mali na kutokana na wimbi lake kuendelea kushika kasi, watendaji wakuu wa serikali wamepaza sauti wakitaka vyombo vya dola kuwaleta katika mkono wa haki washukiwa wake.
Rais Samia Suluhu Hassan kupitia makamu wake wa Rais Dk Philip Mpango, ametoa muda wa siku saba wale wanaotajwa kuwa mauaji hayo yamekuwa yakiripotiwa karibu maeneo mengi nchini na tukio lingine linaloendelea kujadiliwa hivi sasa ni la watuhumiwa wawili wanaodaiwa kutekeleza mauji katika nyumba moja ya kulala wageni jijini Dar es salaam.
Watuhumiwa hao wanadai kukodiwa na mkazi mmoja aliyewalipa ujira wa fedha kwa ajili ya kumua dada aliyedaiwa ni mpenzi wake. Video inayosadikika kurekodiwa na askari inaonyesha jinsi ya mmoja wa watuhumiwa hao akikiri kutekeleza mauaji hayo.
Kumekuwa na maswali mengi yanayoendelea kuibuka kuhusiana na kuongezeka kwa matukio hayo ya kikatili, lakini Bupe Mwambenga ambaye ni mtaalamu wa saikolojia anasema kuwa.
Ongezeka la wimbi la mauwaji sasa linaonekana kuwa kama donda ndugu na mwananchi wameanza kupata hisia mpya hasa baada ya matukio ya hivi karibuni kuwahusisha pia maafisa wa jeshi la polisi waliotiwa mbaroni kwa tuhuma za kumua mfanyabiashara mmoja mkoani Mtwara wakitaka mali zake.
George Njogopa