1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yabadilisha mfumo wake wa ellimu

Deo Kaji Makomba
2 Novemba 2023

Serikali ya Tanzania imetangaza maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ili kutoa elimu ya ujuzi badala ya elimu ya taaluma pekee ambapo elimu ya lazima itakuwa ya miaka 10 badala ya saba kama ilivyo sasa.

Kassim Majaliwa, Premierminister von Tansania
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Picha: Büro des Premierministers von Tansania

Kauli ya serikali ya Tanzania imetolewa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Kassim Majaliwa wakati akitoa taarifa kuhusu kuidhinishwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023 na Mitaala ya Elimu ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema utekelezaji wa maboresho hayo utaanza mwaka 2027 sambamba na kufuta mtihani wa darasa la saba na badala yake kuanza kufanyika kwa tathimini darasa la sita kwa ajili ya kujiunga na elimu ya lazima ya sekondari.

HRW: Wasichana waliofukuzwa shule kwa sababu ya kupata mimba Tanzania wateseka

Aidha Waziri mkuu Majaliwa amezitaja changamoto nyingine kuwa ni Mitaala kutokidhi mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia, mfumo usio fanisi wa udhibiti na ithibati ya elimu na upungufu wa nguvu kazi, huku Changamoto hizo zikizaa hitaji la kuboresha sera ya elimu ili kukidhi mahitaji ya sasa na wakati ujao.

Mabadiliko ya Elimu yanadiwa kufanyika wakati muafaka

Wanafunzi wa shule ya msingi ya New Life mjini Arusha, Tanzania Picha: Veronica Natalis/DW

Mabadiliko hayo ya sera ya elimu nchini Tanzania, yanatajwa na wadau wa elimu nchini humu kuwa yamekuja wakati muafaka kutokana na kiu iliyokuwepo muda mrefu ya kutaka kufanyika mabadiliko ili vijana wanaopitia katika taasisi za elimu kuanzia ngazi ya chini hadi elimu ya juu, wanapohitimu elimu yao waweze kupambana na mazingira yanayowazunguka. 

Tanzania na mfumo mpya wa elimu

Hatua hiyo ya serikali ya Tanzania imefikiwa baada ya kubainika kwa changamoto mbalimbali zikiwemo, mfumo wa elimu kujikita zaidi kwenye elimu ya jumla na kukosa fursa za elimu na mafunzo kwa kuzingatia mahitaji na njia mbalimbali za ufunzaji kutokidhi kulingana na mazingira.

Mwandishi: Deo Kaji Makomba/DW Dodoma

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW