1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yafuzu kushiriki AFCON 2025

20 Novemba 2024

Timu ya kandanda ya Tanzania Taifa Stars imefuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025.

Mshambuliaji wa Taifa Stars Simon Msuva aliyefunga bao la ushindi.
Mshambuliaji wa Taifa Stars Simon Msuva aliyefunga bao la ushindi.Picha: Sia Kambou/AFP/Getty Images

Hii ni baada ya kuifunga Guinea 1-0 katika mechi ya kusisimua iliyochezwa Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao la ushindi na la kipekee limefungwa na mshambuliaji Simon Msuva kunako dakika ya 61. Burundi ilishindwa kufuzu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Senegal mjini Dakar.

Tanzania inaungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda ambazo ni timu za ukanda wa Afrika Mashariki zilizofuzu kushiriki michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika  itakayoandaliwa nchini Morocco mwaka ujao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW