1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kutoa chanjo ya Covid-19 kwa umma

5 Julai 2021

Tanzania  imetangaza rasmi kuwa nchi hiyo imekwisha kamilisha mwongozo wa kupokea na kutunza chanjo za Covid 19 ili kutoa fursa kwa wananchi wenye uhitaji wa kuchomwa chanjo dhidi ya virusi hivyo,

Tanzania Daressalam Fahrgäste mit Mundmasken
Picha: DW/S. Khamis

Wakati Wizara ya Afya nchini Tanzania  ikitangaza rasmi kuwa nchi hiyo imekwisha kamilisha mwongozo wa kupokea na kutunza chanjo za Covid 19 ili kutoa fursa kwa wananchi wenye uhitaji wa kuchomwa chanjo dhidi ya virusi hivyo, itakayotolewa bure, hisia mseto zimeibuka kutoka kwa watu wa makundi mbalimbali huku wakiitaka serikali kuwa makini na watu wenye nia mbaya ya kuingiza chanjo bandia.

Tahadhari hiyo ya wananchi kwa serikali ya Tanzania, imetolewa huku kukiwepo na taarifa katika nchi jirani ya Uganda kuwa tayari watu wapatao 800 nchini humo wanadaiwa kupewa chanjo bandia ya Covid 19 na hivyo kuzusha wasiwasi na mashaka miongoni mwa watu waliokwisha chanjwa nchini humo.

Wasiwasi wa baadhi ya wakazi kuhusu kitisho cha chanjo bandia umeanza kuzungumziwa.

Chanjo aina ya Sputnik V ya inayotengenezwa UrusiPicha: Kirill Kukhmar/TASS/dpa/picture alliance

Wakizungumza na DW kutoka katika maeneo tofauti nchini Tanzania, baadhi ya watu wamesema, hakuna tena namna, ni lazima Tanzania iendane na matakwa ya jumuiya ya kimataifa kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19 ikiwemo chanjo, lakini serikali katika nchi hiyo imetakiwa kuwa makini na watu wenye nia ya kutaka kuingiza chanjo bandia. Selemani Msindi ni mkaazi wa mkoani Morogoro anasetoa rai ya kudhibitiwa chanjo bandia.

Wasiwasi wa baadhi ya watu nchini Tanzania kuhusiana na uwezekano wa baadhi ya watu kuingiza chanjo bandia unazidi kuwepo miongoni mwa watu huku wakiitaka serikali kuendelea kutoa elimu ya kutosha kuhusiana na chanjo hizo ili kujenga uelewa kwa wananchi. Bwana Maguye Simon ni mkaazi wa Morotonga wilayani serengeti mkoani Mara kaskazini Magharibi mwa Tanzania anahimiza mikakati madhubuti ya usalama wa chanjo.

Tanzania imeonesha nia ya kuzalisha chanjo yake yenyewe kwa kupunguza gharama.

Tayari serikali ya Tanzania kupitia katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Abeli Makubi imesema kuwa  hatua mbalimbali na madhubuti zinaendelea kuchukulia ili kudhibiti wimbi la tatu la Covid 19 ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha chanjo ili kuzalisha chanjo hizo ndani ya nchi, kutoa elimu kwa jamii  kuhusu janga hilo na kuongeza kuwa.

Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imeruhusu chanjo ya ugonjwa corona kusambazwa bure katika taasisi za umma na binafsi huku ikitoa mwongozo wa kujikinga na ugonjwa huo katika taasisi za elimu.

Chanzo: DW Dodoma

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW