1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yapiga marufuku maandamano ya Desemba 9

9 Desemba 2025

Serikali ya Tanzania imeonya kwamba maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumanne ni kinyume cha sheria na yatachukuliwa kama jaribio la mapinduzi, huku ikiwataka wananchi kusalia majumbani mwao.

Dar es Salaam | Serikali na Polisi wapiga marufuku maandamano ya Desemba 9, 2025
Wanaharakati wameitisha maandamano Desemba 9, 2025 kudai mageuzi na hakiPicha: Eric Boniface/DW

Polisi imesema maandamano yamepigwa marufuku kwa kuwa mamlaka haikupokea taarifa yoyote rasmi kutoka kwa waandaaji huku kauli hiyo ikisisitizwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania George Simbachawene.

Ulinzi umeimarishwa sehemu mbalimbali hasa katika miji mikubwa kwa kuenezwa vikosi vya polisi na wanajeshi waliojihami kwa silaha. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuondolewa kwa marufuku hiyo  na kuvitaka vyombo vya usalama kutotumia nguvu kupita kiasi katika kudhibiti maandamano hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW