1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Tanzania yashitakiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Veronica Natalis
14 Novemba 2025

Mashirika manne ya kutetea haki za binadamu Tanzania, yamefungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali ya Tanzania. Ikipinga sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta.

Tanzania | Rais Samia Suluhu
Rais Samia Suluhu Hassan wa TanzaniaPicha: AP/picture alliance

Shauri hilo limefunguliwa na mashirika manne ya kutetea haki za binadamu nchini  Tanzania ambayo ni  kituo cha sheria cha haki za binadamu LHRC, Baraza la habari Tanzania MCT, Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC pamoja na taasisi ya Center for strategic litigation, na vifungu vinavyolalamikiwa ni pamoja na kile kinachozuia uhuru wa kutoa na kupokea taarifa, na kwamba baadhi ya vifungu havijafafanua kwa uwazi dhana ya makosa ya kusambaza maudhui.

Mawakili upande wa mashitaka ambao ni wakili Jeremia Mtobesya na Wakili Peter Manjanjala wamevitaja vifungu vyenye utata kuwa ni pamoja na kifungu namba tatu, nne, tano na sita, pamoja vifungu vingine kadhaa vya sheria hiyo yaEPOCA kwamba vinakiuka mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuitaka Mahakama itamke kuwa vifungu hivyo ni batili.

Sheria hiyo ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta, pamoja na mambo mengine inatoa adhabu ya faini ya shilingi milioni tano, au kifungo cha miezi 12 kwa ambaye atatiwa hatiani kwa makossa ya kimaudhui, mawakili hao wakisema adhabu hiyo ni kubwa mno na iminya uhuru wa watu kutoa maoni yao kwenye mitandao.

Tanzania: Tumerekebisha vifungu vinavyolalamikiwa

Hata hivyo mawakili upande wa serikali ya Tanzania wakiongozwa na Wakili Stanley Kalokola wakati wakijibu hoja za waleta maombi, wameieleza mahakama hiyo kuwa vifungu vingi ambavyo vinalalamikiwa tayari vimefanyiwa marekebisho na serikali. Godfrey Kamenge ni mchambuzi wa masuala ya haki za binadamu.

Mahakama ya Afrika Mashariki imeeleza kuwa itapanga siku ya kutoa maamuzi baada ya shauri hilo baada ya kukutana na mawakili waliofungua kesi pamoja na mwanasheria mkuu w serikali ya Tanzania. 

Rais Samia:Haki kwa watuhumia izingatiwe

04:06

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW