Tanzania yasitisha mitandao ya gazeti la Mwananchi
3 Oktoba 2024Moja ya video ya katuni iliyotolewa mtandaoni mapema wiki hii na The Citizen ilionyesha Rais Samia Suluhu Hassan akitazama kanda za habari za wapinzani na wahanga wa ukandamizaji wa serikali.
Gazeti hilo tayari lilikuwa limeondoa matangazo hayo ya uhuishaji, likisema katika taarifa tofauti kwamba "zilionyesha matukio ambayo yaliibua wasiwasi kuhusu usalama na usalama wa watu binafsi nchini Tanzania".
Soma pia:Rais wa Tanzania aamuru uchunguzi visa vya utekaji na mauaji
Gazeti la The Citizen, mojawapo ya magazeti yenye ushawishi mkubwa kwa lugha ya Kiingereza, lilitoa taarifa siku ya Jumatano likisema machapisho yake ya mtandaoni yamesitishwa kwa siku 30 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu na serikali za Magharibi, ikiwemo Marekani, wamekosoa kile wanachokiona kama ni ukandamizaji upya kabla ya uchaguziwa serikali za mitaa mnamo Novemba na uchaguzi mkuu mwishoni mwa 2025.