1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yatangaza kudhibitiwa kwa homa hatari ya Marburg

Prosper Kwigize2 Juni 2023

Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani WHO imetangaza rasmi kudhibitiwa kwa homa hatari ya virusi vya Marburg vilivyoripotiwa mwezi Machi mwaka huu na kugharimu maisha ya watu kadhaa katika mkoa wa Kagera.

Tansania | Ummy Mwalimu | Gesundheitsministerin
Picha: Prosper Kwigize/DW

Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu ameutangazia ulimwengu kuhusu kudhibitiwa na kumalizika kwa virusi vya homa ya Marburg ambavyo viliripotiwa mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania na kusababisha vifo vya watu sita kati ya tisa waliobainika kuwa na maambukizi.

Kufuatia kupatikana kwa mafanikio hayo Waziri Mwalimu ameshukuru jumuiya ya kimataifa hususani Umoja wa Ulaya, Marekani na Umoja wa Afrika kwa kutoa misaada mbalimbali iliyotumika katika mapambano hayo ikiwemo kutoiwekea vikwazo nchi hiyo.

Miongoni mwa watu watatu walionusurika kifo baada ya kuambukizwa Marburg ni Mganga wa kituo cha Maruku Dr. Mahona Ndalu mbaye ametoa ushuhuda wa kilichompata.

Dr. Tumaini Nagu mganga mkuu wa serikali akitoa taarifa ya athari za mlipuko wa homa ya marburg ambapo watu tisa waliambukizwa na watatu kupoteza maisha huku wengine zaiďi ya 200 wakipata athari za kijamii, kuchumi na kisaikolojiaPicha: Prosper Kwigize/DW

Watu watano wafariki Tanzania baada ya mripuko wa homa ya Marburg

 Ni wapi ugonjwa huu ulitoka?

Swali hili linamuumiza Waziri wa afya Ummy Mwalimu pamoja na hivyo kulazimika kutoa wito kwa watafiti wa ndani na nje kufanya uchunguzi wa kina.

Shirika la Afya duniani kupitia kwa mwakilishi wake nchini Tanzania Dr. Zabron Yoti wametoa pongezi kwa Tanzania kwa namna serikali ilivyochukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzuia maambukizi kutosambaa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla.

Taarifa ya serikali ya Tanzania imebainisha kuwa pamoja na watu tisa walioambukizwa na vifo vya watu 6, watu wengi zaidi waliathirika kwa namna mbalimbali na mripuko huo.Picha: Science Photo Library/IMAGO

Pamoja na hayo Umoja wa Afrika na chake cha udhibiti wa magonjwa Africa CDC kupitia kwa kaimu mkurugenzi wake nchini Tanzania Dr. Ahmed Ogwell Ouma pamoja na kupongeza kwa namna nchi za Afrika zinavyoshirikiana, amehimiza nchi za Afrika Mashariki kuwa na mpango wa pamoja wa kushughulikia magonjwa ya milipuko.

Ugonjwa wa Marburg umewahi kuikumba nchi ya Uganda kwa mara saba katika nyakati tofauti na kufanikiwa kuudhibiti hali inayoziamsha taasisi za utafiti kufuatilia kwa kina kuhusu chanzo cha ugonjwa huo.

Mwandishi: Prosper Kwigize- DW Bukoba Kagera

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW