1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yazindua daraja refu la Tanzanite

24 Machi 2022

Daraja jipya la kisasa linalokatiza kandokando ya bahari ya hindi katika jiji la Dar e salaam nchini Tanzania limezinduliwa huku kukiwa na matumaini ya kupungua foleni katika jiji hilo la kibiashara. 

Tanzania Dar es Salaam | Tanzanite Brücke
Picha: Tanzania President Press

Daraja hilo linalofahamika kwa jina la Tanzanite linaonekana kubadili sura ya jiji la Dar es salaam ingawa baadhi ya wakosoaji wanasema kuwepo katika eneo hilo hakuwezi kuwa suluhisho la moja kwa moja la kupunguza kero ya foleni.

Likijengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa ushirikiano na serikali ya Korea Kusini, daraja la Tanzanite limejiambaza pembezoni kidogo mwa kitovu cha jiji na mwenekano wake ni kivutio tosha cha jiji hili la bandari.Samia apokea ripoti ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi

Rais Samia akizindua daraja la TanzanitePicha: Tanzania President Press

Limeanzia kando kidogo mwa ufukwe wa habari ya hindi ambako liko daraja la salenda na kuambaambaa pembezoni mwa bahari hiyo hadi sehemu iliko maskani mwa makazi ya mabalozi wengi wa kigeni.

Eneo ambako daraja hilo linakomea ni sehemu ambako ni maskani mwa watu wa kipato cha juu kama vile maeneo ya Osterbay, Masaki na Mikocheni. Kumekuwa na maoni mengi kuhusiana na daraja hilo kama linaweza kuwa suluhisho la kumaliza foleni inayoshuhudiwa zaidi nyakati za asubuhi na jioni.

Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu na DW

This browser does not support the audio element.

Ingawa hakuna majibu ya moja kwa moja kuhusiana na hoja hiyo, hata hivyo serikali inaamini kuwa kuwepo kwake kumesaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa adha hiyo ya foleni.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makala anasema daraja hilo siyo tu kwamba linajibu swali kuhusu tatizo la foleni, bali pia ni taa inayomulika muonekana mzuri wa jiji hili.

Mtendaji mkuu wa wakala wa barabara(Tanroads), Mativila Rogatusi amesema daraja hilo limejengwa na serikali kupitia mkopo nafuu wa serikali ya Korea Kusini. Rais Samia Suluhu Hassan ndiye anayezindua daraja hilo ambalo linatajwa kuwa refu zaidi nchini Tanzania. Daraja hilo ni moja ya vivutio vinavyolipendekezesha jiji la Dar es salaam ingawa kumekuwa pia na daraja lingine la Kigamboni ambalo pia linakatiza bahari ya Hindi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW