Taratibu mpya za uwekezaji katika Bundesliga
27 Machi 2015Matangazo
Kanuni mpya iliyofichuliwa na wasimamizi wa ligi hiyo, inapunguza zaidi uwezekano wa kuwepo na uwekezaji mkubwa katika ligi hiyo.
Shirika linaloidhibiti Bundelsiga, DFL, limekubaliana kuhusu tatibu hizo mpya zinazofanya iwe vigumu kwa wawekezaji wanaotaka kununua vilabu. Hivi karibuni, wahusika wa tatu ambao ni makampuni ya kitaifa na watu binafsi wataruhusiwa tu kuhusika katika idadi ya juu ya vilabu vitatu pekee, na hawataruhusiwa kumiliki zaidi ya asilimia 10 ya hisa katika mojawapo ya vilabu hivyo.
DFL imesema taratibu hizo zimechukuliwa kwa ajili ya kile imesema ni „kulinda uadilifu na uaminifu wa ushindani wa michezo“.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu