1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tatizo la kufariki watoto wadogo wakati wa uzazi.

13 Juni 2005

Ripoti ina asema linaweza kupungua tu iwapo hatua kabambe zitachukuliwa, ili kufikia lengo ya milenia.

Ikiwa maendeleo barani Afrika katika inayoonekana hivi sasa , eneo la bara hilo la kusini mwa jangwa la Sahara litaweza kufikia malengo la milenia ya Umoja wa mataifa ya kupunguza vifo vya watoto wakati wa uzazi, sio ifikapo 2015 kama inavyokusudiwa bali karne moja baadae. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti na ripoti yake kuwasilishwa na Mkurugenzi wa Shirika la mpango wa maendeleo la umoja wa mataifa Kevin Watkins katika mkutano uliofanyika mjini Berlin.

Ripoti hiyo mpya inachambua juu ya hali katika sekta kama , vifo vya watoto ,umasikini na elimu . Wataalamu wa maendeleo wanasema ili malengo hayo yafikiwe, sio tu ni muhimu kwamba Viongozi wa nchi nane tajiri, wanaongeza fedha za misaada kwa ajili ya shughuli za maendeleo, bali pia wanatoa haki za kibiashara na kuwaondolea mzigo wa madeni wenye madeni makubwa. Nchi hizo nane pamoja na hayo wamepiga hatua upande huo , walipokutana mawaziri wao wa fedha mwishoni mwa juma lililopita mjini London.

Viongozi wa dunia walikubaliana juu ya malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2000. Hayo yanakusudia kufikia hatua kubwa ya maendeleo ifikapo 2015, ikiwa ni pamoja na katika masuala kama kupungua kwa theluthi mbili idadi ya watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa, kuzuwia kusambaa kwa ugonjwa wa Ukimwi, haki sawa baina ya wanaume na wanawake, na elimu ya msingi kwa wote.

Lakini Bw Watkins anasema kama hali itaendelea kuwa kama ilivyo sasa , kwa mtazamo wa maisha yanayopotea na nguvu za binaadamu barani Afrika, gharama itakua kubwa mno. Takwimu alizoziwasilisha ni mkondo ambao unaweza kubadilishwa kwa kubadilika sera za kitaifa pamoja na ushirikiano imara zaidi wa kimataifa.Lakini kama hali itaendelea kuwa kama ilivyo, watoto milioni 19 bado watabakia bila ya elimu kufikia 2015 katika eneo la jangwa la Sahara-inasema ripoti hiyo.

Eneo hilo la Afrika lina asili mia 37 ya jumla ya watoto 115 milioni ambao hawaendi shule, na idadi yake inaweza ikaongezeka. Baadhi ya nchi kama Tanzania, Kenya, uganda na Rwanda zimepiga hatua ya maendeleo katika kuwaorodhesha watoto kwa ajili ya elimu ya msingi, lakini zinabakia nyuma katika kukamilisha malengo hayo.

Kundi la nchi za G8 zikiwemo saba zilizoendelea kiviwanda ni pamoja na -Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Itali, Japan na Marekani- na pia Urusi. Viongozi wa nchi hizi watakutana kwa mkutano wa kilele huko Scotland-Uingereza mwezi ujao, na jumuiya kadhaa zimetoa woito kutaka maamuzi makubwa zaidi yachukuliwe kuhusu suala la maendeleo katika nchi masikini.

Tilmann Brück, mtaalamu wa masuala ya maendeleo katika taasisi ya utafiti wa kiuchumi ya Ujerumani, anasema anaona kuna hatua nne muhimu zinazopaswa kuchuliwa na Viongozi wa mataifa hayo tajiri. Hizo ni kuongeza msaada wa maendeleo, kupunguza au kufuta madeni, kukubali paweko na haki za kibiashara kwa wote na kumaliza migogoro.

Amedokeza kwamba karibu nusu ya bajeti ya Umoja wa ulaya inafidia wakulima na kupunguza mtindo huo, kutatoa mchango mkubwa kabisa katika msaada wa maendeleo. Lakini Rais Jacques Chirac wa Ufaransa aliwaambia waandishi habari mjini Paris Ijumaa iliopita kwamba hayuko tayari kufanya mabadilikliko yoyote katika utaratibu huo wa kufidia wakulima miongoni mwa mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Ripoti inasema nchi za kiafrika kusini mma jangwa la sahara zinaweza zikashindwa kufikia lengo la kupunguzwa umasikini kwa nusu ifikapo 2015. Kwa mujibu wa makadirio ya Umoja wa mataifa kiasi ya watu 353 milioni katika eneo hilo watakua watakua katika umasikini mkubwa-ikiwa ni 219 milioni zaidi ya idadi ya hii leo. Hiyo itakua na maana kwamba hata kiwango cha umasikini katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kitapanda kutoka 29 asili mia hadi 53 asili mia .

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW