Tbilisi. Serikali yavunjwa, waziri mkuu afutwa kazi.
17 Novemba 2007Matangazo
Rais Mikhail Saakashvili wa Georgia amemuondoa madarakani waziri mkuu Zurab Nogaideli pamoja na serikali yake, na kumteua kiongozi maarufu wa benki kuchukua nafasi yake. Hatua hiyo inaonekana ya kujipigia debe kuweza kushinda uchaguzi kabla ya uchaguzi uliotishwa kwa dharura hapo Januari 5. Wakati huo huo wizara ya mambo ya ndani ya Georgia imesema kuwa imeondoa amri ya hali ya hatari iliyowekwa baada ya ghasia kuzuka katika mitaa ya Tbilisi. Wabunge wa Georgia wamepiga kura siku ya Alhamis kuondoa amri hiyo ya hali ya hatari , ambayo rais Mikhail Saakashvili aliamuru hapo Novemba 7, baada ya maandamano makubwa kumtaka kujiuzulu kumalizika kwa mapigano na jeshi la usalama.