1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tedros: Mizozo duniani yabezwa, kisa wanaoteseka si weupe

14 Aprili 2022

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameilaumu jumuiya ya kimataifa kwa kuelekeza nadhari zaidi juu ya vita vya Ukraine.

Kuwait | WHO Generaldirektor Tedros Adhanom Ghebreyesus
Picha: Jaber Abdulkhaleg /AA/picture alliance

Tedros amehoji kuwa mizozo kwingineko, ikiwemo katika taifa lake la nyumbani Ethiopia, haipewi uzingativu sawa, yumkini kwa sababu wale wanaoteseka siyo weupe.

Sijui kama ulimwengu unayazingatia kwa usawa maisha ya watu weusi na weupe. Nilisema wiki iliyopita, nadhari yote kwa Ukraine ni muhimu sana pasina shaka, kwa sababu inaathiri dunia nzima. Lakini sehemu yake ndogo tu haitolewi kwa Tigray, Yemen, Afghanistan, Syria na kwingine. Sehemu tu.

Tedros alikuwa anazungumza katika mkutano wa vidio kutokea Geneva jana Jumatano. Mwezi uliyopita Tedros alisema hakuna popote duniani, ambako afya ya mamilioni ya watu inakabiliwa na kitisho kikubwa kuliko mkoa wa Ethiopia wa Tigray, akidai kuwa malori 20 tu ya msaada ndiyo yemeruhusiwa kuingia mkoani humo tangu kutangazwa kwa mapatano wiki tatu zilizopita, badala ya takribani malori 2,000.

Hali ya kiutu kaskazini mwa Ethiopia ni mbaya mnoPicha: Alemnew Mekonnen/DW

Tedros amesisitiza kwamba kuna karibu watoto 6,000 wanaoishi na Ukimwi katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, lakini mamlaka zimepoteza mwelekeo kuhusu walipo watoto hao na kwa maana hiyo inahisiwa kwamba wengi wao wamekwishafariki dunia. Ameelezea hali katika jimbo hilo kuwa ni janga, wakati watu wengine wakifa kutokana na kukosa chakula. 

Soma pia: Serikali,Waasi washutumiana kutofika misaada ya kiutu Tigray

Mwezi uliopita, Tedros ambaye aliwahi kuwa waziri wa afya wa Ethiopia alisema hakuna mahali kwenye ulimwengu huu ambako watu wake wanakabiliwa na kitisho kikubwa zaidi ya hali ilivyo kwenye jimbo hilo la Tigray.

Kote kaskazini mwa Ethiopia, mzozo huo wa miezi 17 umesababisha zaidi ya watu milioni mbili kukimbia makazi yao, kwa mujibu wa Umoja wa Maatifa na kuwaacha zaidi ya watu milioni tisa wakihitaji msaada wa chakula. Umoja wa Mataifa unaiita Yemen mzozo mbaya kabisa wa kibinaadamu kuwahi kutokea ulimwenguni. Aidha umoja huo unatafuta ufadhili kwa ajili ya Afghanistan, ambayo iko ukingoni mwa kuporomoka kiuchumi, huku zaidi ya watu milioni 24 wakihitaji msaada wa kiutu ili kuishi.vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka Syria mwaka wa 2011 na karibu watu nusu milioni wameuawa na mamilioni kuwachwa bila makaazi katika mzozo huo

Reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW