1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: I ran yaonya kuhusu azmio la Umoja wa Mataifa

31 Julai 2006

Wizara ya mambo ya kigeni ya Iran imeonya kuwa Teheran haitoshughulika na mapendekezo yaliyotolewa na nchi za magharibi kuhusu mradi wake wa kinuklia,ikiwa siku ya Jumatatu,Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapitisha azimio dhidi ya Iran.Hayo ni matamshi rasmi ya kwanza kutolewa na Iran kuhusu mswada wa azimio,unaoipa Iran nafasi hadi mwisho wa mwezi Agosti,kusita kurutubisha madini ya uranium au itakabiliwa na kitisho vikwazo vya kimataifa.Mswada huo usiotoa mwito wa moja kwa moja kuchukua hatua ya vikwazo, huenda ukapigiwa kura mapema leo Jumatatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW