1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Iran yaionya Israel

24 Julai 2006


Rais Mahmoud Ahmadnejad wa Iran amesema Israel imebonyeza kifungo cha maangamizi yake kutokana na hatua inazochukua nchini Lebanon.

Rais Ahmadnejad pia amerudia kauli yake ya mwaka jana juu ya kuwataka waisrael wafunge virago na waondoke.

Kiongozi huyo wa Iran ametoa kauli hiyo kujibu madai ya Israel kwamba nchi yake inahusika na kutekwa wanajeshi wawili wa Israel,kisa ambacho kimesababisha mgogoro wa sasa wa mashariki ya kati.

Iran imekanusha madai hayo.

Israel pia imeilaumu Iran kwa kuwapa wapiganaji wa Hezbollah fedha na silaha.

Bwana Ahmadnejad amesema anawashauri waisraeli wafunge virago na waondoke mashariki ya kati kabla ya kukumbwa na moto waliouwasha wao wenyewe.

Wakati huo huo Syria imesema kwamba itaingia katika vita vya Lebanon ikiwa majeshi ya Israel yatakaribia mpaka wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW