TEHERAN: Uchaguzi wa rais
17 Juni 2005Matangazo
Wananchi karibu milioni 46 wa Iran wametolewa mwito wa kujitokeza ili kumchagua rais wa nchi yao.
Wakati huo huo hatua kadhaa zimechukuliwa kwa lengo la kuimarisha usalama nchini kote kufuatia mashambulio ya mabomu ya hivi karibuni.
Aliyekuwa rais hapo zamani bwana Akbar Hashemi Rafsanjani anatazamiwa kuwa na matarajio makubwa ya kushinda.Watu wengine sita pia wanagombea kiti hicho cha urais.
Rais George Bush wa Marekani ameukosoa uchaguzi huo nchini Iran na kusema kwamba siyo wa haki.
Bwana Bush ameeleza kwamba Iran inatawaliwa na watu wanaokandamiza uhuru ndani ya nchi na kueneza ugaidi nchi ya nchi.
.