TEHERAN : Wapalestina wamehidiwa msaada wa pesa na Iran
12 Desemba 2006Matangazo
Iran imeahidi kutoa msaada wa Dola milioni 250 kwa serikali ya waziri mkuu wa Wapalestina,Ismail Haniyeh,inayoongozwa na chama cha Hamas.Haniyeh alitoa taarifa hiyo wakati wa ziara yake ya siku nne nchini Iran.Amesema,Teheran imepanga kuipa serikali ya Kipalestina dola milioni 120 katika mwaka 2007 na vile vile italipa mishahara ya watumishi wa serikalini katika wizara tatu,kwa miezi sita ijayo.Pesa hizo zitaziba pengo la misaada ambayo Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya zilisita kutoa kwa Wapalestina,baada ya chama cha Hamas kushinda uchaguzi na kushika madaraka mapema mwaka huu.