1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran: Harakati za kidiplomasia za Uturuki kuhusu mzozo wake na Iraq

28 Oktoba 2007

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki, Ali Babacan, leo alisisitiza kwamba nchi yake inawacha wazi uwezekano wa kuchukuwa hatua za kijeshi dhidi ya wapiganajii wa Kikurd walioko kaskazini mwa Iraq, na akaitaka jamii ya kimataifa iiunge mkono zaidi nchi yake. Ali Babacan alisema, baada ya kufanya mazungumzo na waziri mwenzake wa Iran. Manouchehr Mottaki, kwamba Uturuki ina njia tafauti za kuchukuwa, inaweza kutumia njia za kidiplomasia au za kijeshi, na njia zote hizo zinazingatiwa. Alisema wananchi wa Uturuki wanaishiwa na subira, na wanataka marafiki zao wawaunge mkono katika juhudi zao za kupigana na ugaidi.

Naye Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, katika mazungumzo ya simu na wenzake wa Iraq na Urturuki, aliwalaumu magaidi wa chama cha Wakurd cha PKK wanaofanya harakati zao kutokea Kaskazini mwa Iraq, akisema magaidi hao si marafiki wa nchi yeyote.

Pia waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameyalaumu mataifa ya Umoja wa Ulaya kwa kutochukuwa hatua zaidi kupambana na harakati za chama cha Wakurd cha PKK, akisema nchi hizo za Ulaya haziwakamati na kuwakabidhi wanachama wa PKK kwa Uturuki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW