1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran yashutumiwa kwa kutaka kuwa na silaha za kinuklia.

13 Novemba 2005

Maafisa wa Marekani na wa mataifa ya Ulaya wanasema kuwa ushahidi mpya unaashiria kuwa Iran inatafuta kuwa na silaha za kinuklia. Madai hayo yanakuja wakati Iran imekataa pendekezo lililotolewa kwa pamoja na Ujerumani , Ufaransa na Uingereza ambalo linaitaka Iran kutuma madini yake ya Uranium nchini Russia ili yakarutubishwe huko.

Maafisa wa Iran wanasema kuwa nchi hiyo inapaswa kuwa na uwezo wa kuzalisha fueli zake za kinuklia.

Nchi hiyo inakabiliwa na hatua ya kuipeleka katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa ajili ya uwezekano wa kuwekewa vikwazo baada ya kushindwa kuwaishawishi jumuiya ya kimataifa kuwa nia yake ya kuwa na nishati ya kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW