1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN. Iran yataka kuendelea na mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia na umoja wa Ulaya.

6 Mei 2005

Iran imesema inataka kuendelea na mazungumzo kuhusu mpango wake ya nishati ya nuklia pamoja na umoja wa Ulaya. Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Kamal Kharzai, amewaambia waandishi habari mjini New York, kwamba nchi yake ina utayarifu wa kuyaendeleza mazungumzo hayo ili mradi kunayo matumaini ya kuyafikia makubaliano.

Iran imekubali kusitisha kwa muda shughuli zake zote za kuyarutubisha madini ya uranium, lakini imetishia kuzirudia tena shughuli hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW