1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran yataka majadiliano zaidi na umoja wa Ulaya.

27 Agosti 2005

Mjumbe wa Iran katika majadiliano ya kinuklia Ali Larijani amesema kuwa nchi yake inampango wa kutoa mapendekezo mapya kuhusiana na mazungumzo ya kinuklia na nchi za Ulaya katika muda wa mwezi mmoja.

Taarifa yake inafuatia mkutano na kiongozi wa shirika la kimataifa la Nuklia Mohammed el Baradei mjini Vienna.

Larijani amesema kuwa Iran haijaondoa uwezekano wa majadiliano zaidi na umoja wa Ulaya , hata kama umoja huo umesitisha mazungumzo ukipinga dhidi ya hatua ya Iran ya kuanza tena kazi ya kuchuja fueli za kinuklia.

Hata hivyo, Larijani ameongeza kuwa kitisho cha kuiwekea vikwazo Iran katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusiana na mpango wake wa kinuklia hakijaiweka nchi hiyo katika hali ya wasi wasi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW