1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yawaruhusu wachunguzi wa umoja wa mataifa

7 Novemba 2005

Iran imekubali kuwaruhusu wachunguzi wa umoja wa mataifa kuchunguza mpango wake wa nyuklia. Maofisa wa ngazi za juu nchini humo wanasema serikali ya Tehran inataka kuanza mazungumzo na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani juu ya mpango wake wa nyuklia.

Barua ya mpatanishi mkuu wa Iran katika mzozo huo wa nyuklia, anayetaka kuanza tena kwa mazungumzo hayo, imepelekwa kwa mabalozi wa mataifa hayo matatu ya umoja wa Ulaya. Marekani inailaumu Iran kwa kujiandaa kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Iran inasisitiza mpango wake huo ni wa kuzalisha umeme.

Iran imethibitisha kwamba jana iliwaruhusu wachunguzi wa umoja wa mataifa kuitembelea kambi ya jeshi ya Parchin, na kufanya mazungumzo na maofisa wakuu, kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na madai ya Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW