TEHRAN: Naibu kiongzi wa shirika la IAEA aitembelea Iran
11 Julai 2007Matangazo
Naibu wa kiongozi wa shirika la kimataifa la kuzuia utapakazaji wa silaha za kinyuklia, IAEA, Olli Heinonen, amewasili nchini Iran hii leo kw aziara inayolenga kuutanzua mzozo wa nyuklia wa Iran.
Ziara ya kiongozi huyo inafanyika siku chache baada ya shirika la IAEA kutangaza kwamba Iran imepunguza shughuli zake za kurutubisha uranium.
Lakini ujumbe wa shirika hilo ulipowasili mjini Tehran, rais wa Iran, Mahmoud Ahmedinejad, amesema nchi yake haitasitisha urutubishaji wa madini yake ya uranium.
Maafisa wa Iran pia wamesema Heinenon hataruhusiwa kuchunguza kinu chohcote cha nyuklia nchini humo, ikiwa ni pamoja na kinu cha Natanz ambako urutubishaji wa uranium unafanywa.