1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Rais Bashar al-Assad wa Syria ziarani Iran

17 Februari 2007

Rais Bashar al-Assad wa Syria amewasili mji mkuu wa Iran,Tehran.Wakati wa ziara hii ya siku mbili atakutana na rais mwenzake Mahmoud Ahmadinejad, mkuu wa dini wa Iran-Ayatollah Ali Khamenei na rais wa zamani,Akbar Hashemi Rafsanjani.Mada zinazotazamiwa kupewa umuhimu mkubwa ni Irak, Lebanon na ushirikiano pamoja na Wapalestina.Iran na Syria zina uhusiano wa karibu tangu Ahmedinejad kushika madaraka.Nchi hizo mbili zinatuhumiwa kuwa zinawasaidia waasi katika nchi ya jirani Irak.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW