1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaapa kujibu vitisho vya Trump, Hormuz

22 Machi 2026

Iran imesema itaishambulia miundombinu ya nishati na mitambo ya kuchuja majichumvi katika eneo la Ghuba ikiwa Marekani itailenga miundombinu ya nishati ya nchi hiyo.

Iran  Ghuba ya Uajemi | Kitalu cha mafuta cha Soroush
Vituo vya nishati kote kwenye eneo la Ghuba vimelengwa wakati wa vita, hali inayoongeza bei ya gesi na mafuta duniani.Picha: IMAGO

Marekani na Iran zinatishia kuvizidisha vita vyao, kwa kulenga vituo vya nishati hali ambayo itayumbisha zaidi masoko ya nishati na fedha duniani na wakati huo huo kuzidisha mgogoro wa kikanda.

Rais wa Marekani Donald Trump, ameonya kwamba nchi yake itaishambulia na kuiharibu kabisa miundombinu ya nishati ya umeme iwapo Jamhuri hiyo ya kiislamu haitoufungua mlango bahari wa Hormuz katika muda wa saa 48. Tamko la Trump amelitoa siku moja tu baada ya kuzungumzia kuhusu "kuvimaliza" vita, ambavyo sasa viko katika wiki yake ya nne.

Meli ya mafuta pembezoni mwa bandari ya Sultan Qaboos, Muscat, OmanPicha: Stelios Misinas/REUTERS

Iran ilionya Jumapili kwamba itailenga miundombinu ya Marekani, ikiwemo ya nishati katika eneo la Ghuba, ikiwa Trump atatekeleza vitisho vyake, ambavyo alivitoa huku Wanajeshi wa Marekani na vifaa vya kijeshi vikielekea katika eneo la Mashariki ya Kati.

Zaidi ya watu 2,000 wameuawa mpaka sasa tangu Marekani na Israel zilipoanzisha vita dhidi ya Iran mnamo Februari 28. Vita hivyo vimeathiri masoko ya biashara, vimeongeza gharama za mafuta na kuchochea hofu ya mfumuko wa bei duniani na pia vimeuathiri Muungano wa Magharibi ulioundwa1945 baada ya vita unaoongozwa na Marekani unaounganisha Ulaya Magharibi na Amerika Kaskazini kupitia taasisis kama vilejumuiya ya kujihami ya NATO.

Mchambuzi wa masoko ya Hisa Tony Sycamore, amesema Iran ikivilenga vituo vya nishati kwenye nchi za Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Qatar, hatua hiyo bila shaka itaongeza maumivu kwa kupandisha bei ya nishati na kuziingiza nchi hizo katika mgogoro mpana wa kikanda.

Amesema mashambulizi ya Iran yamesababisha kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, eneo jembamba linalopitisha takriban theluthi moja ya gesi asilia duniani na mafuta, na kufungwa kwake kumesababisha mgogoro mbaya zaidi wa mafuta tangu miaka ya 1970 na kupanda bei za gesi barani Ulaya hadi asilimia 35 wiki iliyopita.

Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Nathan Howard/REUTERS

Mchambuzi wa masoko ya Hisa Tony Sycamore, amesema wazo la Trump kuhusu kuishambulia Tehran kutokana na kuufunga mlango bahari wa Hormuz ni kwa ajili ya kuiadhibu na kuidhoofisha Iran kiuchumi na kisiasa.

Trump na utawala wake wanatoa ujumbe mchanganyiko kuhusumalengo ya Marekani katika kipindi chote cha vita, hatua hiyo inawachanganya washirika wa Marekani wakitafuta majibu bila kuyapata.

Kura mpya ya maoni ya Reuters/Ipsos, iliyofanywa wiki iliyopita, imebaini kuwa asilimia 59 ya Wamarekani hawakubaliani na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran, huku asilimia 37 wakiwa wanaunga mkono vita hivyo.

Vita hivyo vimekuwa dhima kubwa ya kisiasa kwa Trump kabla ya uchaguzi wa bunge wa katikati utakaofanyika mwezi Novemba, huku ongezeko la bei ya nishati likichochea mfumuko wa bei nchini Marekani na kuwaathiri vibaya biashara pamoja na watumiaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW